Nina virusi vya ukimwi lakini mpenzi wangu hajui-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Mwanamume adai mpenzi wake hajui kama ana virusi vya ukimwi
Teke Teke:Mbusi na Lion
Image: Studio

Ukidhani umeyasikia yote unapata bado hujayasikia, jinsi wanawake wanapitia magumu bila ya kujua.

Mwanamume mmoja alitoboa siri na kusema kwamba ana virusi vya ukimwi bali mpenzi wake hajui na wamekuwa wakifanya tendo la ndoa kwa muda.

Huku akiendelea na simulizi yake, alisema kwamba ameambukiza wanawake wengine watano virusi hivyo, ambapo mmoja ana mtoto wake.

 

"Nataka kutobolea mpenzi wangu siri kwamba, niliambukizwa ukimwi na mwanamke lakini ameshaaga dunia

Baada ya yake kuaga nilipatana na mpenzi ambaye niko naye sasa lakini hajui kama nina virusi vya ukimwi, nimekuwa nikisafiri kutoka ncho moj hadi nyinge kwa ajili ya kazi, kwa huvyo hatukai sana naye

Tumekuwa tukifanya tendo la ndoa tukipatana lakini hatutumii kinga kwa maana ananiamini, licha hayo yote kuna wanawake wengine ambao nimefanya nao ngono lakini sijui kama niliwaambukiza

Kuna mmoja wao ambaye ana mtoto wangu, nataka kutoboa hii siri ili aweze kuenda hospitali akapimwe, ndio aendelee na madawa kama mimi," Mwanamume huyo alisimulia.

Je ni chuki kipi mwanamume huyo ako nayo ambapo hangemwambia mpenziye kama kwa kweli anampenda?