Dada yangu anajua niko Dubai lakini niko kenya-Mwanamke atoboa siri

Muhtasari
  • Ni siri ipi ambayo umefungia moyoni mwako na unataka jamii,ijue au wataka kuitoboa?
  • Haya basi usitie shaka kwani unafursa ya kuitoboa katika kipindi cha Mbusi na Lion teketeke, engi wamekuwa wakitoboa siri huku wakimwaya mtama
Teke Teke:Mbusi na Lion
Image: Studio

Ni siri ipi ambayo umefungia moyoni mwako na unataka jamii,ijue au wataka kuitoboa?

Haya basi usitie shaka kwani unafursa ya kuitoboa katika kipindi cha Mbusi na Lion teketeke, engi wamekuwa wakitoboa siri huku wakimwaya mtama.

Mwanamke mmoja siku ya JUmatano alisimulia jinsi dada yake anafahamu yuko nchi za nje ilhali yko kenya na watoto wawili na mume.

 

Huu hapa usimulizi wake;

"Dada yangu alinisomesha tangu wazazi wangu waage dunia, nilimaliza kidato cha nne mwaka wa 2017

Nilipata alama ya C+, baada ya kumaliza rafiki ya dada yangu alimwambia kwamba kuna wafanyakazi ambao wanahitajika Dubai

Aliniambia nijisajili niende, nilijisajili, lakini baada ya wiki moja nilipigia mwanamume huyo na kumwambia kwamba sitaki kuenda Dubai

Nilitoka kwa dada yangu Nakuru nikaenda Nairobi kuolewa, sasa nina mume na watoto wawili, lakini dada yangu anajua kwamba niko Dubai nafanya kazi,

Nataka kumtobolea siri kwamba niko kenya na wala siko Dubai kama vile anavyofikiria" Alisimulia mwanamke huyo.