Baba yangu ni mpenzi wa dada ya mpenzi wangu-Mwanamke atoboa siri

Muhtasari
  • Mwanamke atoboa siri jinsi alimpata baba yake na mwanamke mwingine

Katika kitengo cha toboa siri, na watangazaji wao uwaoendao Mbusi na Lion, mwanake mmoja alitoboa siri jinsi alipatana na baba yake siku ya wapendanao mwaka huu akiwa ameenda kujivinjari na mwanamke mwingine.

Sio mwanamke tu bali ni dada ya mpenzi wake, kwani mpenzi wake alikuwa amempeleka wakajivinjari siku hiyo maalum.

Kulingana na mwanamke huyo alitaka kumtobolea baba yake siri hiyo, ili wawachane na dada ya mpenzi wake.

"Ilikuwa siku ya wapendanao mwaka huu, ambapo mpenzi wangu aliamua kunipeleka 'out' mahali tulienda ama klabu ambayo tulienda nilimuona baba yangu akiwa na mwanamke mwingine wakijivinjari lakini nikajifanya sijawaona

Cha kushangaza ni kuwa mpango huyo wa kando au mpenzi huyo wa baba baba yangu ni dada yake mpenzi wangu

Amekuwa akija kwetu na kujifanya kwamba ni rafiki yangu,kumbe kuna jambo anaendeleza na baba yangu

Nataka kumtobolea baba yangu siri hii kwamba mwanamke aliyenaye, na mpenzi wake ni daa ya mpenzi wangu na wanapaswa kuachana," Alisema mwanamke huyo.