Mama wa kambo wangu ana mimba yangu-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri jamaa alitoboa siri na kuweka wazi kuwa mama yake wa kambo ana ujauzito wake na wala sio wa baba yake
  • Ni swali ambalo limesalia bila ya majibu, licha ya watu kuwa na maswali chungu nzima
Lion,DJ Nyce na Mbusi
Image: Studio

Katika kitengo cha toboa siri jamaa alitoboa siri na kuweka wazi kuwa mama yake wa kambo ana ujauzito wake na wala sio wa baba yake.

Ni maajabu ya kushangaza ambayo yanashuhudiwa kila kuchao nchini, lakini swali kuu ni nani wa kulaumiwa kwa vitendo hivi.

Asilimia kubwa ya watu wengi wanasema kwamba miandao ya kijamii na baadhi ya filamu ndio za kulaumiwa, pia kuna wale wanadai kwamba wazazi wanapaswa kulaumiwa kwa kuto wafunza watoto wao.

Ni swali ambalo limesalia bila ya majibu, licha ya watu kuwa na maswali chungu nzima.

Huu hapa usimulizi wa mwanamume huyo;

"Baba yangu alioa mke wa pili amabye ni mama yangu wa kambo,hii ni baada ya mama yangu kutoka kwa ndoa kwa maana alikuwa anpenda pombe sana

Baba yangu anaishi nairobi nasi tunaishi mashambani, nataka kutoboa siri na nimwambie kwamba ujauzito ambao mama wa kambo ameubeba sio wake bali ni wangu," Alisimulia.