Niliacha kuenda kanisa kwa maana pasta ana deni yangu-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa asema aliacha kanisa kwa sababu pasta hajamlipa deni lake

Katika kitengo cha toboa siri mwanamume aliwatobolea washirika wa kanisa ambalo alikuwa anaenda siri kwanini alikoma kuenda katika ibaada.

Kulingana na mwanamume huyo aliacha kuenda kanisa baada ya kumkopesha pasta wa kanisa hilo pesa na kukataa kumlipa.

"Niliokoka mwaka jana baada ya kuchukua mshahara wangu pasta wa kanisa ambalo nilikuwa anaenda aliniomba elfu tatu,

Kabla ya hapo alikuwa ameniambia nitoe fungu la kumi lakini sikuwa na pesa, bilipomuitisha pesa zangu alianza kuongea vibaya kisha nikaamua kutoka kwa kanisa

Nataka kuwatobolea washirika wa kanisa hilo ambao wamekuwa wakiniuliza mbona siendi kanisani, ni kwa ajili ya pasta aliongea vibaya nilipomuitisha deni yangu,"

Ndio huwa tunawaona watu wengi wakijikakamua na kuenda kanisani, lakini baada ya muda mfupi  wanaacha huku wengi wakisalia na maswali kwanini waliacha kuenda kanisani.

Kuna baadhi ya wahubiri ambao huwa wanawafukuza wahsiriki wao kwa matendo yao wenyewe bila ya kujua haswa wamewakosea.