Niliharibu uzazi wangu baada ya kujitahiri-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Mwanamume mmoja aliwashangaza wengi baada ya kutobia siri jinsi aliharibu uzazi wake baada ya kujitahiri akiwa na miaka 19
Mbusi na Lion

Wakishindwa kuyaweka moyoni, haya basi huwa wana mwaya mtama kwenye kipindi cha Mbusi na Lion teketeke katika kitengo cha toboa siri.

Mwanamume mmoja aliwashangaza wengi baada ya kutobia siri jinsi aliharibu uzazi wake baada ya kujitahiri akiwa na miaka 19.

Sababu ya kujitahiri

"Nilijitahiri nikiwa na miaka 19, hii ni baada ya baba yangu kukataa kunipa pesa za kutahiri, nilitumia tu wembe wa kawaida, sikujua kwamba nimekata mshia wa maana wa uzazi

Hata nikifanya tendo la ndoa siwezi pata mtoto, wala sina ile hamu , nimejaribu kufanya tendo la ndoa na wanawake tofauti lakini nguvu zangu zinaambulia patupu,"Alieleza Mwanamume huyo.

siri

"Nataka kutobolea mama yangu na dada zangu ambao wamekuwa wakinisukuma ili nipate mtoto lakini hawajui wala kufahamu kwamba siwei kuwa na watoto

Nataka wanajambo wanipe ushauri kama naweza tembelea mtaalam,"

Je ni ushauri upi utampa mwanamume huyo?