Niliwadanganya marafiki zangu kuwa nafanya kazi Radiojambo kama mtangazaji Mbusi-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa atoboa siri jinsi amekuwa akiwadanganya watu anafanya kazi Radiojambo
Mbusi,Lion na DJ Slim
Image: Studio

Sio mmoja au wawili bali asilimia kubwa ya wakenya wamekuwa wakitoboa siri, baada ya kushindwa kuziwekwa kisha wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri.

Shabiki mmoja kutoka Uganda ametoboa siri jinsi amekuwa akiwadanganya marafiki zake anafanya kazi Radiojambo kama mtangazaji Mbusi.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nikiwa Uganda kuna baadhi ya marafiki zangu waliniuliza kenya nafanya kai gani, niliwaambia kwamba nafanya kazi Radiojambo kama mtangazaji Mbusi

Lakini hawajui kwamba nafanya kazi ya mjengo,nataka kuwatobolea marafiki zangu kwamba nafanya kazi ya mjengo na wala sio radiojambo

Nilikula shilingi elfu mbili za mmjoa wa marafiki zangu,ambapo ni shilingi elfu sabaini pesa za Uganda," Alisimulia.