Alikuwa na nyoka ambao walikuwa wanalalia noti za elfu moja-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri, wengi umwaya mtama na kufichua siri ambazo wamekuwa wakiweka kwa miaka mingi
  • Mwanamume mmoja alieleza jinsi aliajiriwa kazi ya kuosha na kuwapa nyoka chakula

Katika kitengo cha toboa siri, wengi umwaya mtama na kufichua siri ambazo wamekuwa wakiweka kwa miaka mingi.

Mwanamume mmoja alieleza jinsi aliajiriwa kazi ya kuosha na kuwapa nyoka chakula.

Hii hapa siri yake;

"Nilikuwa natafuta kazi nilipatana na mwanamume akanibeba kwa gari lake na kunipeleka nyumbani kwake

Alinipeleka katika chumba kimoja kilichokuwa na giza na kunionyesha nyoka 4 ambao walikuwa katika chumba hicho

Wawili walikuwa wa kiume na wawili wa kike na alikuwa amewapa majina, kazi yangu ilikuwa ya kuwapapasa, kuwaosha na kuwapikia uji

Cha kushangaza ni kuwa nyoka hao walikuwa wanalalia noti ya elfu moja,na walikuwa wakubwa sana, nataka kuwatobolea wanakijiji kwamba wasijaribu kkuenda nyumbani mwa mzee huyo kwani kuna nyoka mkubwa ambaye anaweza kuwala," Alieleza jamaa huyo.

Pia alitaka ushauri wa wanajambo kama alifanya vyema kutoka kwa kazi hiyo au la.

KUlingana naye kama angekuwa hapo angekuwa ameshaakufa.