Niliishi na mpenzi wangu kwa miaka 2 kumbe alikuwa mke wa mtu-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa atoboa siri jinsi aliishi na mke wa mtu bila kujua

Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama, kwani wasipo toboa siri zitawasumbua katika miyo zao.

Je unamfahamu mpenzi wako vyema na unajua kazi ambayo anafanya, na maisha yake ya awali?

Jamaa mmoja alitoboa siri jinsi aliishi na mpenzi wake Kisumu, bila ya kujua kwamba ni mke wa mtu.

Hawakukosea waliposema mke wa mtu 'is a no go zone area'.

Hii hapa siri yake

"Niliishi na mpenzi wangu kwa miaka miwili, kama bibi na bwana nilikuwa naonja maisha ya ndoa, kwa miaka hiyo yote sikufahamu kuwa alikuwa mke wa mwanamume mwingine

Tulipatana kwa duka, hajawahi niambia kwamba aliuwa mke wa mtu,hatukuwa tumebarikiwa na mtoto

Mwishowe alikuja kuniacha na kumrudia mume wake, nataka kumtobolea na kumwambia kwamba nilijua alikuwa mke wa mtu, pia nimtobolee mke wangu ni mwambie nilikuwa nimeoa ilhali nilimwambia sijawahi oa,"