Malimwengu!Nina uhusiano wa kimapenzi na mama mkwe wangu-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Haya basi kuku walikuwa wengi siku ya JUmanne, hii ni baada ya jamaa kutoboa siri jinsi amekuwa na uhusiano wa kimapenzi wa mama mkwe wake
(kushoto)DJ Slim,(kati)Mbusi (kulia) LIon
Image: studio

Haya basi kuku walikuwa wengi siku ya JUmanne, hii ni baada ya jamaa kutoboa siri jinsi amekuwa na uhusiano wa kimapenzi wa mama mkwe wake.

Kulingana na jamaa huyo mama mkwe ndiye alimtambulisha kwa msichana wake, ilhali bibi yakee hajui hayo yote.

"Nina mke na mtoto mmoja, kuna siri ambayo nimekuwa nataka kutoboa, nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama mkwe wangu

Ndiye alinitambulisha kwa mke wangu, yaani msichana wake, lakini akaniambia kuwa uhusiano etu unapaswa kuendelea lakini nisimwambie

Baba mkwe anafanya kazi ya jeshi,ilhali hajui chochote tumekuwa katika ndoa na mke wangu kwa miaka 2

Nataka kumtobolea mke wangu siri nimwambie kwamba nina uhusiano na mama yake, na ananipenda ziadi anavyonipenda," Alitoboa siri jamaa huyo.

Haya ni malimwengu ambayo tumekuwa tukishuhudia kila kuchao,na wala yamewacha kushuhudiwa kwenye filamu.