Mke wangu anajua nafanya kazi kwa Agrovet, lakini nauza panya-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri kazi ambayo anafanya
(kushoto)DJ Naty,(kati) DJ Luzzy(kulia) Mbusi
Image: Studio

Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri kazi ambayo anafanya.

Kulingana na jamaa huyo alitaka kumtobolea mkewe siri kwamba hafanyi kazi ya kuuza dawa za mifugo kama vile alivyomwambia.

Lakini anafanya kazi gani?, hii hapa siri yake;

"Nilimdanganya mke wangu kwamba nafanya kazi wa Agrovet, lakini nataka kumtobolea siri ni mwambie kwamba sifanyi kazi kwenye duka hizo

Nimekuwa nikianya kazi ya kuwauzia wagagnga panya, panya mdogo anatoka shilingi 250 na mkubwa shilingi 500, nimekuwa nikipata pesa kutoka kwa biashara hiyo

Kwa hivyo nataka ajue kwamba pesa ambazo amekuwa akipokea kutoka kwangu ni za kuuza panya wala sio za agrovet," Jamaa huyo alimwaya mtama.

Je ushauri wako ni upi, je aende na panya hao kwa nyumba, au akomboe nyumba nyingine  ya kuwaeka?