Mke wangu amekuwa akijiuza kwa 'streets'-Mwanamume atobolea mashemeji wake siri

Muhtasari
  • Kuku wakiwa wengi huwa wana mwaya mtama kwenye kitengo cha toboa siri, mwanamume mmoja ametoboa siri jinsi alimpata mkewe akijiuza yaani akifanya kazi ya ukahaba

Kuku wakiwa wengi huwa wana mwaya mtama kwenye kitengo cha toboa siri, mwanamume mmoja ametoboa siri jinsi alimpata mkewe akijiuza yaani akifanya kazi ya ukahaba.

Kulingana na mwanamume huyo, alimchukua baby mama wake kutoka kwa 'streets' na kuahidi kwamba atabadili tabia yake.

Sababu kuu ya kuwa kahaba alisema ni mwanawe.

Hii hapa siri yake;

"Nilipachika mama wa mtoto wangu mimba akiwa kidato cha pili, kisha nikamuacha baada ya miaka 5 nilimpata kwenye streets akijiuza

Nilimtoa huko, kwa maana alidai kwamba alikuwa anafanya hayo kwa ajili ya mtoto wangu baada ya corona nilisimamishwa kazi na sikuwa na uwezo wa kumtimizia mahitaji yake

Alikuwa ananiambia kwamba anaenda saluni lakini amekuwa akienda kufanya kazi ya ukahaba, nataka kuwatobolea mashemeji wangu ni waambie kwamba msichana wao sio mzuri

Na hajakuwa akinifanyia mambo mazuri, amekuwa akifanya hivyo sasa kwa miezi 6, pia nataka ushauri kutoka kwa wanajambo, kama nimtobolee siri kwamba najua amekuwa akifanya kazi hiyo."

Ushauri wako wa jamaa huyo ni upi?