Nilinyakua mpenzi wa baba yangu,nimempachika mimba-Jamaa amwaya mtama

Muhtasari
  • Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama, jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo na mjadala mkali baada ya kufichua jinsi alivyo mtendea baba yake
DJ Gregg,Mbusi na Lion
Image: Studio

Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama, jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo na mjadala mkali baada ya kufichua jinsi alivyo mtendea baba yake.

Jamaa huyo alitoboa siri, jinsi alivyo nyakua mpenzi wa baba yake, siku chache baada ya baba yake kumleta nyumbani.

"Nataka kumtobolea baba yangu siri kwamba, nimechukua mke wake ambaye alimuacha nyumbani

Si hayo tu sasa hivi ana ujauzito wangu wa wiki mbili, alitoka nyumbani na ninaishi naye kwangu, pia nilikuwa namtaka amwambie baba yangu kwamba yeye ni mke wangu

Baba yangu yuko Kakuma, najua majirani wamesikia siri hii watamwambia, kwa ufupi nimenyakua mpenzi wa baba yangu," Jamaa huyo alisimulia.

Je ni ushauri upi unaweza mpa jamaa huyu?