'Sina uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito,nilimhonga daktari atoe ripoti bandia,'Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja alikiri kwamba hana uwezi wa kumpa mwanamke ujauzito
  • Kulingana na mwanamume huyo, alienda kupimwa ili kujua haswa nani ana shida kati yake na mkewe
Image: Studio

Katika kitengo cha toboa siri, jamaa mmoja alikiri kwamba hana uwezi wa kumpa mwanamke ujauzito.

Kulingana na mwanamume huyo, alienda kupimwa ili kujua haswa nani ana shida kati yake na mkewe.

"Nilioa mwaka wa 2012, na miaka hiyo yote hatujaweza kubarikiwa na mtoto, nilienda hospitali mara ya kwanza ili nijue nani haswa ana shida kati yangu na mke wangu

Ripoti zilionyesha kwamba siwezi mpa mwanamke ujauzito, si kumwambia mke wangu chochote mara ya pili mke wangu alinisisitiza niweze kuenda naye hospitali tukapimwe

kwa maana nilijua ni mimi nina shida, nilimhonga daktari abadili ripoti ambapo ziliweza tokea sisi sote tuko sawa

Nataka kutobolea familia yangu hii siri kwamba ni mimi nina shida na wala sio mke wangu kwa hivyo waache kumsumbua na kumtesa,"Alieleza jamaa huyo.

Jamaa huyo anataka ushauri wako afanya aje?