'Wacha kunipigia simu nimeolewa,'Kipusa amtobolea mpenzi wake siri kwamba ameolewa

Muhtasari
  • Kipusa amtobolea mpenzi wake siri kwamba ameolewa
Image: Studio

Kuku wakiwa engi wanamwaya mtamba katika kitengo cha toboa siri, mwanamke mmoja amewaacha shabiki wa radiojambo midomo wazi  baada ya kufichua jinsi amekuwa akimcheza mpenzi wake.

Kwa mujibu wa mwanake huyo, licha yake kuolewa, alipatana na mwanamume mwingine na kumdanganya kwamba hajaolewa na kwa ni pwani ilhali kwa ni Nakuru.

Hii hapa siri yake;

"Nataka kumtobolea mpenzi wangu au mpango wangu wa kando kwamba nmeolewa, nilipata naye miaka 3 iliyopita

Kabala ya kupata naye nilikuwa nimeolewa, ilhali mume wangu alikuwa anaishi Nairobi nami Nakuru, nikienda kumtebelea mume wangu nimekuwa nikimdanganya kwamba naenda Mombasa kuona wazazi wangu

Nataka kumtobolea siri nimwambie nimeolewa na awache kunipigia simu," Alieleza mwanamke huyo.