'Mimi sikupendi, na ujauzito nilionao sio wako,'Kipusa amtobolea mpenzi wake siri

Muhtasari
  • Katika kipindi cha toboa siri siku ya JUmatatu, kipusa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo midomo wazi baada ya kumtobolea mpenzi wake siri

Kweli ya Mungu ni mengi ya kuku ni mayai tu, wadau  niliwaambia kuwa kuwaamini hawa 'daughters of Jezebel' kama  wanavyojulikana mitaani ni kama kupanda mbegu mahali haziwezi mea.

Katika kipindi cha toboa siri siku ya JUmatatu, kipusa mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo midomo wazi baada ya kumtobolea mpenzi wake siri.

Hii hapa siri yake;

"Nataka kumtobolea mpenzi wangu siri, kwamba ujauzito nilionao wa miezi sita sio wake, na kwamba simpendi

Najua anaskiza radiojambo, lakini ajue tu natarajia mtoto wa mwanamume mwingine na ujauzito wenyewe ni wa baba ambaye ni mzee, na amekuwa akinitimizia vyema mahitaji yangu ya kitandani," Alisema kipusa huyo.

Pia alitaka ushauri je aendelee na mpeni wake au aende kuishi na baba wa mtoto wake.