Kati ya 28 hao 24 ni wakenya ilhali 4 ni raia wa Tanzania . wagonjwa 10 ni kutoka Mombasa ,9 Nairobi 4 Migori ,2 Kajiado na kisa kimoja kutoka kaunti za Machakos ,Kiambu na Homabay . Katika jiji la Nairobi ,visa 9 vilivyripotiwa vilipatikana katika mitaa ifuatayo;3 Embakasi,2 Kayole,1 Huruma ,1 South B na kisa 1 Kawangware . Umri wa watu walioathiriwa ni kati ya miaka 11 na 81 . 17 ya waliopatiakana na ugonjwa huo ni wanaume ilhali 11 ni wanawake .
Katibu wa utawala wa wizara ya Afya Rashid Aman amesema mtu mmoja zaidi ameaga dunia na kufikisha 30 idadi ya watu ambao wameaga dunia hadi kufikia sasa . watu wengine 5 wamepona virusi hivyo na kufikisha 207 idadi ya waliopona ugonjwa huo .
Aman amesema makundi ya maafisa wa afya kutoka wizara ya afya yametumwa katika kaunti za mipakani ili kuzisaidia kaunti hizo kukabiliana na virusi vya corona baada ya ongezeko la idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huo katika maeneo ya mipakani .
Kaunti ya Mandera imenufaika na msaada wa wizara ya afya wa kuwafanyia watu vipimo vya corona kabla ya matokeo kuletwa jijini Nairobi kwa tathmini .