Visa 38,000 vya maambukizi ya Corona vyaripotiwa Afrika

NA NICKSON TOSI

Kufikia sasa, visa vya maambukizi katika bara la Afrika vinaendelea kuongezeka huku shirika la afya duniani WHO, likiripoti kuwa watu 38,000 wameambukizwa kufikia sasa.

Vile vile kulingana  na WHO, watu 1600 wameaga dunia kufikia sasa.

Mataifa ya Afrika Kusini, Morocco ndiyo yanayoongoza katika idadi za maambukizi huku taifa la Algeria likiwa linaongoza kwa idadi ya vifo 450.

Tazama jedwali

Tanzania sasa inaongoza na idadi kubwa ya maambukizi ikiwa na 480, ikifuatwa karibu na Kenya ambayo ina visa 396.