Visa 4 vipya vya COVID-19 vimeripotiwa, idadi yafika 42- Mutahi Kagwe

Kuna visa 4 vipya vya COVID-19, waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza.

Wanne hao mmoja ni Mkenya na wageni watatu kutoka Marekani, Cameroon na Burkina Faso.

Vipimo 69 vimeangaziwa kwa kina.

Jumamosi visa 7 vipya vilitangazwa huku idadi ya walioathirika ikifika 38.

Hata hivyo, mgonjwa mmoja aliaga dunia alhamisi. Jamaa huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 66,aliaga katika hospitali ya Aga Khan na alikuwa na ugonjwa wa kisukari.

Hili lamaanisha kuwa Kenya imerekodi visa 37 vya COVID-19. Mtu mmoja amepona tayari.

Visa vyote vilitoka kaunti ya Nairobi.

Kati ya saba hao, Wanne ni wakenya, wawili kutoka Congo na mmoja kutoka Uchina.