Vita dhidi ya COVID-19; wahudumu wa afya 11,000 wapewa mafunzo maalum kuhusu virusi

MWANGANGI
MWANGANGI

Kenya kufikia sasa imewapa mafunzo takriban wahudumu wa afya 11,000 kote nchini kushughulikia janga la COVID-19.

Katibu msimamizi wa afya Mercy Mwangangi siku ya Jumatatu alisema kwamba wahudumu wa afya 60,000 wamepewa mafunzo ili kuimarisha uwezo wa idara ya afya kuimarisha huduma za afya kote nchini.

Mwangangi alisema mafunzo hayo yalilenga sana uhamasisho kuhusu virusi vya corona, maambukizi na hatua za kudhibiti maambukizi.

Alisema wizara yake imepokea msaada wa vifaa vya kusaidia wagonjwa kupumua kutoka kwa shirika la UASID na vifaa hivyo vitasamabzwa kwa kaunti konte nchini.

Mwangangi alisema kwamba tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya corona Kenya ilikuwa na vituo viwili pekee vya kupima virusi vya corona lakini kufikia sasa vituo hivyo vimeongezeka hadi 25.

Kulingana na katibu huyo msimamizi kuongezeka kwa vituo hivi kumepiga jeki uwezo wa Kenya kupima idadi kubwa ya watu.

Alionya dhidi ya dhana kwamba Kenya ni salama na kwamba kama taifa tayari tumekwepa mtengo wa virusi hivyo akisisitiza kuwa maambukizi yanaendelea kusambaa.