Vita dhidi ya Unyanyapaa! Wakenya jasiri waliokiri kuishi na Virusi vya Ukimwi

Ukwimwi ni moja wapo ya magonjwa ambayo yana tisha ulimwenguni na yafaa kutangazwa kama mojawapo ya janga ulimwenguni.

Watu wengi sana wana aga dunia kila siku kutokana na ugojwa huu. Kulingana na ripoti ya WHO ya mwaka wa elfu mbili kumi na saba, kadiria watu 670 000 - 1 300 000 wanakufa kwa Ukimwi duniani kwote.

Kulingana na repoti ya mwaka wa elfu mbili kumi na saba, takriban watu milioni 1.5 Kenya wanaishi na ukimwi na wengi hufa kwa virusi.

Ila tuna watu mashujaa ambao hawaogopi kuweka wazi kuwa wana virusi hivi, kwani kuwa na virusi hivyo haimaaniishi kuwa umefungwa kifungo cha kifo.

Kati ya watu mashuhuri hapa Kenya waliokiri kuwa wanaishi navirusi vya ukumwi ni;

Binyavanga Wainaina

Mwandishi mashuhuri, mtetezi wa haki na mwanaharakati wa mashoga huyu akiweka wazi hali yake ya Ukimwi mwaka wa elfu mbili kumi na sita. Alifanya hivyo kupitia mtandao wake wa Twitter huku akiongezea kuwa alikuwa mtu mwenye furaha.

Mwanzishi  huyu wa Kwani Trust aliandika kwenye Tweeter, ''nina virusi vya Ukwimwi na nina furaha.''

Januari tarehe kumi na nne mwaka wa elfu mbili kumi na nne, Binyavanga alikuja wazi kwa ulimwengu kuhusu hali yake. Alipiga dunia teke mwezi wa Mei tarehe ishirini na moja mwaka wa elfu mbili kumi na tisa baada ya kupooza.

Alitarajiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa Naijeria.

George Barasa alias Joji Baro

Mwanamziki huyu wa nyimbo za injili anaishi na virusi vya HIV.

Katika mahojiano ya awali, Joji Baro aliweka wazi kuwa aliingilia ushoga baada ya kujiunga na shule ya sekondari (St. Paul's Miluki).

Alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na padri wa Kikatoliki ambapo alikuwa ndiye rafiki wa kike.

Mwezi wa Machi mwaka wa elfu mbili kumi na moja, majaribio yake ya ukimwi yalitoka yakiwa chanya. Tangia hapo familia yake ilimpinga na kumuacha ajitegemee.

Phenny Awiti 

Mwandishi huyu wa habari wa Nairobi alikuja wazi kuwa ana virusi vya Ukimwi huku akiwaacha wengi wakishangaa.

Mama ya watoto wawili, wasio na virusi, alisema kuwa baada ya kuweka wazi hali yake, baba ya watoto wake alimuacha.

Phenny, ambaye amekuwa akijenga ufahamu kuhusu virsi vya HIV na akipigia kampeini jamii yenye unyanyapaa bure, aliongezea kwa wanaume ambao walikuwa wamejaa kwenye meseji zake wakimualika chai walitokomea mbali.

Frigacy

George Kihara, mwanamziki wa wimbo Mapenzi ambayo alivuma nayo aligonga vichwa vya habari mwaka wa elfu mia mbili kumi na tatu.

Mwaka mmoja baadaye, Frigacy aliaga kwa mazingira tatanishi.

Tazama wimbo wake hapa

Doreen Moracha

Doreen ambaye ana miaka ishirini na saba alizaliwa na virusi vya ukimwi. Ni mwenye ujasiri na amekuwa akijichikua filamu na kuonyesha ulimwengu safari yake ya kila siku akiwa na Virusi vya ukwimi.

Kama mwenzake, Phenny, Doreen anatumia mitandao yake ya kijamii kuweka fahamu kuhusu ugonjwa huu. Anawahimiza wanaoishi na ugonjwa huu na kuwafunza vijana  jinsi ya kujikinga.

Pia yuko mstari wa mbele kupiga vita dhidi ya unyanyapaa na ubaguaji wa waadhiriwa wa virusi.

Kimutai Kemboi

Kimutai ambaye aliambukizwa na mwanamke ambaye alikuwa anamfanyia kazi hayuko tofauti na wenzake. Hana woga wa kunena hadithi yake na huwa anawatia motisha wengi kupitia maongezi yake.

Alikiri wazi kwenye mtandao wa Facebook kuwa alikuwa na virusi vya ukimwi.