Vitu 5 hufai kufanya ukiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi

love.birds
love.birds
Ni ukweli mtupu jinsi wanamuziki Jaguar na zikki walivyoimba na kusema, mapenzi ni bahari lisilo na mwisho kwani kwa wote ambao wako kwenye uhusiano wa kimapenzi na wapendwa wao, wanaelewa msemo huu.

Hivyo basi, Radio Jambo imewaandalia orodha ya vitu vitano ambavyo hufai kufanya unapo kuwa kwenye mashua hii ya mapenzi.

Soma uimarike.

  1. Hufai kuwa mtu wa kumkontroli mpenzi wako.

Nikisema kumkontrol mpenzi wako, ninamaanisha kuwa, hufai kuwa mtu ambaye unataka kujua yote ambayo mpenzi wako anafanya, na endapo mpenzi wako hajafunguka na kukuambia kila kitu anachofanya, utazua vurugu na kuleta shida kwenye uhusiano wenu.

Endapo una mpenzi, unachotakikana kufanya ni kumuacha mpenzi wako awe huru. Si lazima umwombe ruhusa mpenzi wako kila wakati unapotaka kufanya jambo kwani ninaamini nyinyi nyote ni watu wazima na mnajiweza.

2. Katu usijaribu kuamuru mpenzi wako awache kufanya anchopenda kwa sababu yako.

Ni kosa kubwa sana kumfanya mwenzio awache kufanya anachopenda kufanya kwa ajili yako, kwani utakuwa unamshusha mpenzi wako sana.

Uzoefu huu umekithiri katika mapenzi ya watu wachanga na ata kwa wazee kwani, kwa mfano kama mtu amezoea kucheza mpira ama anapenda kutazama mechi za mpira, mara kwa mara, mpenzi wake anaweza muamuru awache kucheza au kutazama mechi za mpira na amini usiamini, mara kwa mara, mambo kama haya huleta vurugu katika uhusiano huu wa kimapenzi.

Wosia wangu ni kwamba, endapo mpenzi wako anapenda kufanya kitu fulani, kuwa mtu wa kwanza wa kumtia moyo, azidi kupenda anachofanya  na mapenzi yenu yatakuwa shwari bila vurugu mara kwa mara.

3. Usifikiri kuwa unaweza kurekebisha tabia ya mwezako.

Mara kwa mara, wapenzi wanapoanza uhusiano wao, huona kila kitu kikiwa sawa na kuona kana kwamba mpenzi wake ni kamili. Hata hivyo, natumai tunajua kuwa hakuna mtu duniani ambaye ni kamili kabisa, kwa hivyo, kila kitu kina dosari.

Hivyo basi, wazo la kurekebisha tabia ya mtu linafaa kutupiliwa mbali kwani, ni vigumu sana kufaulu kurekebisha mtu kama si yeye mwenyewe ameamua kuwa anataka kubadili tabia yake.

Unapotaka kuishi maisha ya mapenzi yasiyo na vurugu kila wakati, jaribu sana kumuelewa mpenzi wako na badala ya kujaribu kugeuza tabia yake, zidi kumpenda kama unaona kuwa unaeza vumilia anachofanya, walakini, kama tabia yake ni tabia ambayo hauwezi ishi nayo, basi, kata kauli na kukata ushirikiano huo kwani ni vigumu sana kubadili tabia ya mtu.

4. Usiwe mtu msiri ama mwongo 

Sote ni binadamu na ninajua kuwa ni vigumu sana kwa binadamu kamili kusema ukweli kila wakati.

Mara kwa mara, watu hudanganya ili waweze kujiokoa kutoka kwenye tatizo lakini, tabia hii ya kudanganya inaweza kuweka uhusiano wako na mpenzi wako matatani.

Vile vile, maji yatazidi unga, endapo utakuwa msiri sana na umfiche mpenzi wako mambo muhimu ambayo unafaaa kujua. Amini usiamini, mpenzi wako akigundua siri hiyo, maji yatazidi unga na uhusiano wenu kuwa na changamoto nyingi.

Hivyo basi, usiwe msiri na jaribu sana kuwa mkweli kwani naamini kuwa, sote twajua kua siku za mwizi ni arobaini na mwisho, utapatikana tu!

5.Usifikiri kuwa, mambo yatakuwa shwari kila wakati

Ni vizuri tujue kuwa hakuna kitu ambacho kinaweza kosa dosari na hivyo basi, wapenzi wanafaa kuelewa fika kuwa, hata katika bahari la mapenzi, mambo huwa hayaendi shwari kila wakati.

Wakati mwingine, mambo huwa hayawi sawa. Vita vitakuwa, na msisahau wahenga walisema, wagombanao ndio wapatanao hivyo basi, endapo kutakuwa na vurugu, mnafaa kuzisuluhisha kama watu wakubwa na mambo yote yatakuwa shwari.

Haya ndiyo tuliyo nayo siku hii ya leo na ni ombi letu kuwa mtafaidika vilivyo.