Vituko ambavyo baadhi ya wanaume walifanya baada ya kuachwa na wanawake

Kuachwa  ama mwisho wa uhusiano wa kimapenzi ni kitu cha kwaida na mabcaho hufanyika kilasiku wakati watu wawili wanapopata ugumu wa kusuluhisha tofauti zao basi kila mmoja anamaua kwamba ni vyema kushika njia yake .Lakini kuna watu wanaume kwa wanawake ambao hupata ugumu sana kukabiliana na heartbreak  na wakati mwingine kufanya vito vya kushangaza . Haya hapa baadhi ya mambo ambayo wanaume walijipata wakiyafanya bada ya kuachwa ama kukataliwa na wanawake

Kujinyonga

John anasema wakati  mpenzi wake wa miaka mitatu alipomuambia kwamba hataki tena uhusiano naye ,hakuwa tena na hamu ya kuishi . Alikata  uamuzi kwamba basi bila yule mwanadada yeye angeutawa uhai wake na  kwa sumu ya panya alijitayarisha kwenda kuinywa ili afariki .kwa bahati nzuri ,rafiki yake mmoja alimpata chumbani mwake akiwa  bila fahamu na  kumkimbiza hospitalini . John ana bahati kwa sababu kuna watu kadhaa ambao hawakuponea kwani alijiua kwa sababu ya kuachwa na  wapenzi wao au kukataliwa

Alijifanya  amepagwa

Eric anasema wakati mwanamke  ambaye walikuwa wamefunga ndoa naye alipochoka na tabia yake ya ulevi  aliamua kuondoka na kurudi kwao . Anasema hakujua la kufanya na jaribio lake kumrai arudi nyumbani kwa ahadi ya kuacha pombe halikufaulu . Aliamua kujitia  uwendawazimu huku akizichanachana nguo zake ,kukataa kula n ahata kulala nje . Jamaa zake mbio walikimbia kumsimulia  mke wake  kwamba  Eric alikuwa amepagawa kwa sababu ya kuachwa naye . Mkewe apolisikia hayo alirejea mbio akihofya kwamba kitendo chake cha kumuacha ndicho kilichomfanya Eric kupotewa  akili .Alirudi na jamaa akaacha pombe

Aliokoka

Benson hakuwa mcha mungu na hakumbuki mara ya  mwisho alipokwenda kanisani .wakati ulimwengu wake uliposimama ni kipindi alichomtongoza msichana mmoja kwa muda mrefu sana na hakuwa akimtaka . Benson alitumia mbinu zote lakini msichana yule hakubadilisha nia . Ndiposa aliamua kuitumia mbinu ambayo ilifanya kazi kwa njia rahisi kama kuzima mshumaa .Aliokoka. kwa kweli ungemuona  amejikwatua shati jeupe  na mkononi kapatakata biblia akienda kanisani kila jumapili ,basi ungempenda hata wewe na hapo ndipo msichana yule alipokubali  kuwa mpenzi wake .

Jamaa alitafuta kazi

Chris  anasema hakuwahi kuwa na   hraka ya kutafuta kazi kwa sababu wazazi wake walikuwa na pesa . Lakini kila uhusiano wake  ulikuwa haudumu  kwa ajili wanawake walimuona kama mtu mvibu na  ambaye hakuwa na msukumo wa kufaulu ama kuafikia lolote .  Alipogundua tatizo hilo Chris alipata kazi na  tangia hapo maisha yake  ya mahusiano yalibadilika na kuwa ya kudumu .

Kwenda kwa kina msichana kila siku

Elvis alipoachwa na  mpenzi wake  alianza kufanya ziara za kila siku kwenda kwa akina  msichana huyo kujaribu kumshawishi warudiane . Kila siku asubuhi au jioni ungemuona akipitapita katika boma la  kina msichana huyo n ahata wakati mmoja njsura apigwe na wanakijiji waliofikiri kwamba ni mwizi . Angekuja asubuhi na mapema na kupiga kambi nje ya lango kuu ,ili kumgonja msichana huyo akienda kuteka maji  ndiposa apate nafasi ya kuzungumza naye . Angemfuata popote alipokuwa akienda akijaribu kujitetea na kuomba msamaha lakini juhudi zake ziliambulia patupu .

 Jamaa alikuwa akilia  kama mtoto

Mwingine aliyefanya jambo la kuwaacha wengi wakiwa wameshangaa ni Jonas .Alipoachwa na  mpenzi wake ,alikuwa akilia kama mtoto usiku wote watu wakishangaa ni kipi kilichomsibu . Kwa siku kadhaa alijifungua nyumbani mwake akibubujikw amachozi na wakati mwingine akilia kwa sauti huku jamaa zake wakionekana kumhurumia na hata wengine  wakitaka kumpeleka hospitalini akifikiri labda alikuwa na tatizo jingine .