Viwango vya maambukizi ya HIV vyapungua Mombasa

Viwango vya maambukizi ya HIV mjini Mombasa vimepungua pakubwa kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 4.1%.

Tathmini za kaunti hiyo zinaonyesha kuwa kuna maambukizi mapya elfu  1,700 kila mwaka huku kwa sasa wati elfu 41 wanaishi na virusi hivyo.

Mkurugenzi wa afya ya umma katika kaunti hio Shem Patta anasema kaunti hio inanuia kupunguza unyanyapaa katika jamii kwa asilimia 50% kupitia kuhamasisha umma.

Ametoa ushauri kuhusu umuhimu wa ntu kujua hali yake na wale wanaoishi na virusi hivyo tayari kuhakikisha kwamba wanatumia dawa za kuppunguza makali za ARV's ambazo zitasaidia kupunguza maambukizi.

Zaidi ya watu milioni mbili huambukizwa virusi vya HIV kila mwaka, kulingana na takwimu za shirika la kitaifa la kuzuia maambikizi ya HIV na maradhi ya zinaa, NASCOP.

Takwimu kutoka kwa taasisi za afya kwenye kaunti ya Mombasa pia zinaonyesha kwamba zaidi ya watu elfu 18 wanapokea matibabu ya kupunguza makali ya virusi hivyo, kati ya hao elfu 17,955 ni watu wazima, 977 ni watoto na 944 ni vijana wanaobaleghe.