Vogue Challenge : Ni Yupi aliyeweza ? Tazama picha za mastaa wa Kenya wakishiriki shindano hili la mtandaoni

Hakuna asiyependa mashindano ya mitandaoni ambayo kila mara huweka  moto  mitandao ya kijamii kote duniani  na Kenya haijaachwa nyuma katika baadhi ya  challenges hizi nyingi .

Maajuzi kumekuwa na Vogue Challenge ambapo akina dada warembo na mastaa Kenya na kote duniani walitumia ukurasa wa kwanza wa jarida la Vogue  kuziweka picha zao ili kuonyesha minato nayo kwa wote .

Challenge hiyo ilianzishwa  na Salma Noor  aliyesema kwamba aligundua watu wengi weusi hawakuwa wamewekwa katika ukurasa wa kwanza na jarida la Vogue .

“ Kilichonivutia sana  kuanzisha hili ni kwa sababu hapakuwa na uwakilishi wa waytu weusi  ,na baada ya kuibuka suala la ubaguzi wa rangi Amerika nilihisi challenge  hii ilifaa kufanywa’ amesema  Salma

Tazama  picha za  celebs  wa Kenya ambao walishiriki challenge hiyo  na ujiamulie ni yupi aliyefaulu kuivuruga ifaavyo .