Vuo za Bahari Hindi, afurushwa Likoni baada ya kutaka kuogelea

UPDATE+Likoni+ferry+accident+recovery+operations
UPDATE+Likoni+ferry+accident+recovery+operations
Jamaa mmoja aliponea kutumbukia na kufa maji katika kivukio cha Likoni wiki hii Jumatano.

Hii ni baada ya mamlaka ya Huduma ya feri kusitisha operesheni za kawaida katika kivukio hicho.

Jombi huyu alitaka kuogelea ili avuke ng'ambo ya pili baada ya kuona anachelewa.

Juhudi zake za kufanya jaribio hilo zilikatishwa ghafla na wapiga mbizi wanaohusika katika zoezi la uokozi Bahari Hindi.

Soma hadithi nyingine:

Tangazo la Huduma ya feri nchini kusitisha shughuli za kawaida ni jambo ambalo lililemaza biashara na usafiri katika kivukio cha Likoni.

Kivukio hiki kina takriban watu laki tatu kila siku huku magari zaidi ya elfu sita yakihesabiwa kuvuka feri ya Likoni.

Aidha, Licha ya idadi kubwa ya watu wanaotumia kivuko hicho, suala la usalama wa raia limeonekana kutiliwa shaka huku kukishuhudiwa visa vya majanga mbali mbali kila uchao.

Soma hadithi nyingine:

Mkasa wa hivi punde umetia wengi hofu kubwa.

Miili ya mama Miriam Kighenda na bintiye wa miaka minne Amanda Mutheu bado haijaweza kutolewa katika bahari Hindi.

Kivukio hiki kina takriban watu laki tatu kila siku huku magari zaidi ya elMswidi kwa jina Volker Bassen alisubiriwa sana kutoa mchango mkubwa katika zoezi hili ila akaambulia patupu.

Soma hadithi nyingine:

 Matumaini ya kupata gari na miili inadidimia kila uchao baada ya taarifa za hali ya hatari Bahari Hindi.

Kina cha Bahari Hindi kina urefu mkubwa zaidi ambao ni kisiki cha kuendesha zoezi hilo.

Ni kwa urefu huu ambapo Cyrus Oguna anapendekeza kutumia roboti kupiga picha na kukusanya data ya hali ilivyo majini.