Sonko

Vurugu, ghasia zashuhudiwa Sonko akijiwasilisha kwa EACC

Vurugu na ghasia zimeshuhudiwa wakati gavana wa Nairobi Mike Sonko alipojiwasilisha katika afisi za tume ya EACC Jumanne.

Iliwabidi polisi kutumia vitoza machozi ili kuwazuia makundi ya watu waliokuwa wakijaribu kuingia eneo hilo kwa fujo.

Sonko alikuwa amealikwa katika eneo hilo ili kujibu madai ya kughushi hati ya kiapo wakati alipokuwa akiwania kiti cha ugavana.

Vurugu hizo zilianza Sonko alipokaidi amri ya kuingi eneo hilo bila gari lake. Alikuwa ameshauriwa kutembea na kuingia afisi hizo.

Polisi walitumia vitoza machozi ili kuwakabili vijana hao waliokuwa wanajaribu kungia.

Sonko alilazimika kutoka eneo hilo, ila akarejea baadaye.

Hatimaye alirejea na kuingia afisi za tume ya EACC huku akiandamana na wakili wake Lydia Kwamboka.

Soma taarifa nyingine :

Raia Wawili Wa Kigeni Wapewa Muda Wa Siku Tatu Kulipa Bili Ya Hoteli

Uhuru Ashambulia Idara Ya Mahakama

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments