Vyakula 6 vinavyoshusha na kudhaoofisha afya yako

1. Soda

Watu wengi hutegemea soda ili kuzima kiu zao. Lakini soda zinahifadhiwa vihifadhi ambavyo vinajulikana kuathiri homoni zako za mwili.

2. Nyama iliyohifadhiwa

Nyama iliyohifadhiwa ni hatari kwa sababu ya njia iliyohifadhiwa nayo.

Kemikali zilizotumika kuhifadi nyama zile ni ikiwemo Nitrate, sodium na nyinginezo ambazo, hufanya nyama kuwa na rangi ya kupendeza, lakini sio nzuri kwa mwili wako.

3. Saladi ya chupa

Saladi zilizohifadhiwa kwa chupa zinaonekana kuwa hazina madhara yeyote, lakini zimejaa maji matamu ya fructose.

Fructose yaweza kuharibu ini.

4. Pombe

Bidhaa nyingine ambayo kuna mjadala mwingi kuihusu ni pombe. Wataalam wanakubali kwamba kunywa kupita kiasi ni hatari.  Pombe yaweza sababisha upungufu wa maji mwilini, kupata uzito, huzuni, shida za ngozi na uharibifu wa ini.

Madhara mengine ya pombe ni ajali barabarani. Waatalum wanashauri unywaji wastani wa pombe kama vile divai nyekundu, ambayo inaaminika kuwongezea afya mwilini. 

5. Mkate mweupe

Nafaka ni muhimu kwa afya bora, lakini nafaka nyeupe hazina thamani yote ya lishe.

Mkate mweupe, hupandisha sukari kwa mwili na pia inaweza sababisha kupata uzito na pia kuupata ugonjwa wa kisukari.

6. Vyakula vya haraka (Fast Foods)

Vyakula vya haraka yaani fast foods, vimejaa mafuta, sukari, chumvi na kemikali zinazozihifadhi. Vyakula hivyo vinaongeza nafasi kubwa ya kupata ugonjwa wa sukari, kuongeza uzito, ugonjwa wa moyo na mishipa, na ugonjwa wa saratani.

Soma mengi