Waathiriwa Wa Mafuta Yaliyotapakaa Koru Wataka KPC Iwape Makao Mengine

Familia zilizoathirika kutokana kutapakaa kwa mafuta ya diesel eneo la Koru, Muhoroni kutokana na wahalifu kufyonza mafuta kutoka bomba la kampuni ya mafuta – KPC wanashinikiza kupewa makaazi mapya.

Hata hivyo, mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kenya Pipeline Joe Sang amesema familia hizo zitaendelea kupata msaada kutoka kwa kampuni hiyo hadi pale halmashauri ya Mazingira, NEMA itakaposafisha eneo hilo na kulifanya kuwa salama kwa binadamu.

Sang amesisitiza kuwa KPC haijapata hasara kubwa kutokana na kufyonzwa kwa mafuta kwa kipindi cha miezi sita.