Wabunge 23 wataka naibu rais Ruto kujiuzulu

RUTO
RUTO
Jumla ya wabunge 23 wamemshtumu Naibu Rais William Ruto kwa kumdharau Rais Uhuru Kenyatta na kumtaka ajiuzulu.

Walisema naibu rais amekuwa akishambulia maafisa wa serikali na kufanya kila jitihada kusambaratisha maafikiano baina ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kuvuruga ripoti ya BBI.

Wanasiasa hao kutoka vyama vya Jubilee, ODM, Ford Kenya, Wiper na Kanu – wengine wao ambao wamekuwa wakimuunga mkono naibu rais – walimshtumu kwa kupiga vita serikali akiwa ndani na kumtaka aondoke.

“Kama hujaridhishwa na uongozi wa rais Uhuru Kenyatta, nakudhubutu ujiuzulu,” Mbunge wa Tiaty William Kamket alisema.

Wabunge hao walikuwa wanajibu mashambulizi ya wanachama wa mrengo wa Tangatanga siku ya Jumanne, dhidi ya waziri wa usalama Fred Matiang’i, katibu wa kudumu wa maswala ya ndani Karanja Kibichu na Inspekta mkuu wa Police Hillary Mutyambai.

Wanasiasa wa mrengo wa Tangatanga walikuwa wamedai kuwa watatu hao walipanga ghasia zilizoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Kibra wakati wa uchaguzi mdogo wiki iliyopita. Ruto pia amekuwa akimshambulia Raila na wafuasi wake wa ODM akidai kwamba walichochea hali tete ili kushinda uchaguzi huo mdongo au kuvuruga maridhiano baina ra raila na Uhuru.

Lakini wabunge wanaowaunga mkono Uhuru na Raila walisema kwamba mashambulizi dhidi ya maafisa wa serikali ni madharua kwa rais – ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuteua maafisa hao. “Wacha kushtumu wafanyikazi wa umma. Wacha kushtumu waziri, katibu wa kudumu na Inspekta mkuu wa polisi. Jitokeze peupe na kusema tu kwamba ni rais unashtumu,” Kamket alisema.

Waliohudhuria mkutano huo katika majengo ya bunge ni Jimmy Angwenyi (Kitut Chache North), Gathoni Wamuchomba (Mwakilishi wa wanawake Kiambu), Ben Momanyi (Borabu), Fatuma Gedi (Mwakilishi wa wanawake Wajir), Peter Mwathi (Limuru), Mishi Mboko (Likoni) and Raphael Wanjala (Budalang'i).

Wengine walikuwa Ken Chonga (Kilifi Kusini), Jerusha Momanyi ( Mwakilishi wa wanawake Nyamira), Abdikarim Osman (Fafi) na Samuel Arama (Nakuru Mjini).

Momanyi ambaye amekuwa mwandani wa Naibu Rais, alibadili msimamo na

kusema wataunga mkono mapendekezo ya BBI kufanyia katiba mabadiliko ili kumpa rais mamlaka kumtimua naibu wake ambaye ni mtovu.“Uhuru anafaa kupewa mamlaka kumfuta naibu wake. Tunataka mabadiliko ya katiba rais akipata naibu rais mwenye utovu wa nidhamu,anaweza kumfuta kazi.

Huezi jifanya wewe ni naibu wa rais na huku unadhalilisha urais,” Momanyi alisema.

Angwenyi, ambaye pia ni naibu kiongozi wa wengi bungeni, pia alikashifu mrengo Tangatanga kwa kutaja jamii gusii kijiji pamoja na kumshambulia waziri Matiang’i.