Wabunge wa Kenya wanalipwa mishahara mikubwa zaidi duniani- IMF, IPSA

Ripoti ya utafiti wa mamlaka huru kutoka Uingereza inayofahamika kama Independent Parliamentary Standard Authority (IPSA) pamoja na shirika la IMF (International Monetary Fund) imeorodhesha wabunge wa Kenya kama wanaolipwa mishahara minono zaidi  duniani wakiwafuata wenzao wa nchi ya Nigeria.

Wabunge wa Kenya wanaingiza mishahara mikubwa  kila mwisho wa mwezi wakilinganisha na wale wa Marekani, Japani na Uingereza.

Idadi kubwa ya wakenya wana maoni kuwa wabunge wamelipwa ya mishahara ya juu  hivi kufanya gharama ya kuendesha miradi ya serikali kuwa muhali.

kati ya idadi ya viongozi hao 416, kila mmoja anapokea takribani milioni 2.25. Kando na hela hiyo, wanapata marurupu ya takriban milioni 5 kama mkupuo wa kununua magari ya kifahari kila kipindi cha miaka 5. Zaidi ya hapo, wanapata kitita cha milioni 7 ya kununua gari na riba ya asilimia 3 kwa mwaka (3%).

Hali kadhalika, wabunge hawa wana marupurupu yao ya kimatibabu pamoja na wapenzi wao na watoto walio chini ya miaka 25.

Marupurupu mengine ni kama bima ya ajali ndogo, usafiri, vikao katika bunge na kamati za bunge.

Hadithi imetafsiriwa na kuhaririwa na Abraham Kivuva