wabunge wa pwani wadai kusalitiwa na ODM

Kundi moja la wabunge kutoka kanda ya Pwani wamekishtumu chama cha ODM kwa kusaliti eneo hilo kuhusiana na mfumo wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti.

Wabunge 10 kutoka kaunti mbali mbali za pwani walitaja maseneta wanne kutoka eneo la Luo Nyanza na kusema ni maadui wa pwani.

Soma habari zaidi;

Wakiongozwa na mbunge wa ODM Owen Baya (Kilifi North), wabunge hao wa Pwani walisema kuwa maseneta hao wakiongozwa na James Orengo (Siaya), Fred Outa (Kisumu), Moses Kajwang’ (Homabay) na Ochillo Ayacko (Migori) kwa kupiga kura kunyima kaunti za pwani raslimali ni usaliti mkubwa.

“Mjadala na hatimaye kupigiwa kura kwa mswada uliowasilishwa na kiranja wa wengi katika seneti Irungu Kangata kufanyia marekebisho mfumo wa ugavi wa mapato ya kitaifa ulidhihirisha marafiki wetu wa kweli," Baya alisema.

Wabunge hao walisema mchakato huo mzima ulionyesha sura halisi ya wenzao katika mrengo wao wa kisiasa.

Soma habari zaidi;

“Maseneta wa ODM walitupa Pwani chini ya basi na kutuacha kwa pembe za upweke ," Baya alisema.

Walisema kwamba hatua hiyo ya maseneta wa ODM itaathiri pakubwa ushabiki wao kwa chama hicho mwaka 2022 wakiongeza kuwa eneo hilo linatafakari kuhusu kupata marafiki wapya.

Wabunge hao walijumuisha Mohammed Ali (Nyali), Michael Kingi (Magarini), Aisha Jumwa (Malindi), Sharif Ali (Lamu East), Andrew Mwadime (Mwatate), Khatib Mwashetani (Lunga Lunga), Jones Mlolwa (Voi) Paul Kahindi (Kaloleni) NA Benjamin Taya (Kinango)

Soma habari zaidi;