Wabunge wataka noti za 1000 kuondolewa mara moja

Kundi moja la wabunge sasa linataka Serikali kupunguza muda wa kuondolewa kwa noti ambazo zimekuwepo za elfu moja. Wabunge hao wapatao 20 na ambao waliandamana na Naibu Rais William Ruto siku ya Jumapili wanataka serikali kuondoa noti hizo kabla ya mwezo Oktoba.

Wabunge hao waliokuwa wameandama na Naibu Rais William Ruo walisema kwamba kutolipwa kwa wafanyibishaa na serikali kumeathiri sana ukuaji wa biashara nchini, hususan biashara ndogo na za kadri.

Walizungumza siku ya Jumapili katika kanisa la Kahawa eneo Bunge la Ruiru walipotaka serikali kutilia maanani maslahi ya wafanyibiashara wadogo.