Ruto

‘Wacha ajue nilifunzwa kunukuu bibilia tangu utotoni,’Ruto amjibu Raila

Vita vya maneno vimeshuhudiwa mara kwa mara kati ya naibu rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga huku vikizidi endapo wawili hao wanazungumza kwenye mkutano wowote.

Ruto mnamo Jumanne alimpa jibu kinara huyo baada ya kusema kuwa Ruto amekuwa akinukuu biblia hata kushinda maaskofu.

Ruto apuuzilia mbali uvumi kuwa Uhuru atasalia mamlakani

Ruto 1

“Wiki iliyopita aliambia watu wa Taita Taveta kuwa DP ananukuu Biblia kuliko hata maaskofu na anapenda kuenda kanisa. Mimi nilifunzwa kuhusu neno

Kama kuna kurasa zimeandikwa kuhusu uganga, basi hiyo mimi sijui. Yeye anaweza kuongea kuhusu hilo. Huyo wachaneni na yeye

Wacha ajue nilifunzwa kunukuu biblia tangu utotoni.” Alizungumza Ruto.

Raila amewaonya viongozi vya kanisa dhidi ya kuchukua msaada wa pesa kutoka kwa naibu rais kwa maana hiyo ni moja wapo ya njia ya ufisadi.

Eliud Owalo ajiunga na kambi ya DP Ruto kabla ya kipute cha 2022

Raila Odinga
Raila Odinga

Kwenye ziara yake ya ukanda wa Pwani, Raila alimfananisha Ruto na mtu mnafiki anayetumia kanisa na mali yake kuwateka wananchi kisiasa.

Hata hivyo, wafuasi wa Ruto wametupilia mbali mishale ya maneno kutoka kwa wakosoaji wake wakisema wanachomwa roho kwa kuwa anaelewa masaibu ya raia.

Photo Credits: maktaba

Read More:

Comments

comments