Mheshimiwa Jaguar ashambuliwa kuhusu mchipuko wa Corona

NA NICKSON TOSI

Wakenya katika mitandao ya kijamii wamemshambulia mbunge wa Starehe Charles Njagua almaarufu kama Jaguar kutokana na usemi wake kuwa China ndiyo iliyosababisha kuwepo kwa Corona ulimwenguni na hivyo inastahili kutupilia mbali madeni ya Kenya.

Mara nyingine Jaguar amenukuliwa akidai kuwa bilioni 650 ambazo Kenya ilichukuwa kutoka Uchina zinastahili kupewa wafanyabiashara wadogo wadogo na wakaazi wa mitaa ya mabanda nchini ambao wameathirika pakubwa na mkurupuko wa virusi vya corona.

Aidha Jaguar alikiri kwamba itakuwa vigumu kwa serikali kuwalizimu watu kukaa makwao hasa wale wanaofanya vibarua na ambao hulipwa kwa siku ili kujipatia kipato cha siku. Alisema kwamba iwapo serikali inapania kuchukuwa hatua hiyo ni sharti iwalishe wananchi wake.

“Virusi vya Corona vilitokea Uchina, nilazima watufutilie mbali madeni yote ya Kenya shilingi bilioni 650, tuwape wafanyibiashara wadogo na wale wanaoishi katika mitaa ya mabanda  pesa hizo, hatuwezi waamrisha watu wanaojituma kila siku eti wasitoke makwao ilhali hawana chakula nyumbani mwao,aliandika Jaguar katika mtandao wake wa Twitter.

Hapa ni ujumbe huo kamili alioutuma Jaguar katika mtandao wake wa Twitter

Baadhi ya wananchi waliousoma ujumbe huo walikuwa na hisia hizi za kusema

 Yani umekaa to chini ukafikiria hivi.. manifesto ya jubilee ilikuwa?

 Hii ndio inaitwa ujinga wa hali ya juu.

 Hapa you have umefikiria kama ule Patrick wa SpongeBob

 Sisi Kama wasee wa Mukuru tumekataa hilo wazo bana!