Wachana na sisi tafuta mpenzi na mpate watoto-Makau Mutua amwambia Dennis Itumbi

Makau Mutua
Makau Mutua
Wakili wa haki za Binadamu Makau Mutua Jumatano kupitia kwenye mitandao ya kijamii walianzisha cheche za maneno na mwanablogu Dennis Itumbi kuhusu uongozi wa Kenya Human Rights Commission (KHRC).

Cheche za maneno zilianza pale Mutua alimpongeza kinara wa chama cha ODM, Raila Odinga baada ya kuunga mkono kuhusu mvumo wa ugavi wa pesa za kaunti.

"Nilijua hakuna niia yeyote Raila Odinga na Moses Kuria wangekuwa katika ukurasa mmoja kuhusu ugavi wa pesa za kaunti." 

Itumbi hakukimya bali alimshauri atoke kuwa mwenyekiti wa KHRC, wizara ilioanzishwa na Mutua tangu 1991.

"Je KHRC kama NGO inaamini katika mapito, ina masharti kwa wana chama wao? ama ni kama Cotu ukichaguliwa na kuwa mwenyekiti utatumika tangu kifo kikutenganishe na kazi yako

Kwa hayo je KHRC huwa wanafanya uchaguzi wao?naona wewe ni mwanachama na mwentekiti wa miaka yote, tafadhali ni elimishe." Aliandika Itumbi.

Makau Mutua alimpa bonge la jibu na kumwambia kuwa amejaribu kupiga vita chama cha KHRC alipokuwa mfanyakazi kazi wa ikulu bali hakuweza kufaulu.

"Dennis mdogo wangu kwanini ujisumbue na KHRC? ulijaribu kupiga vita  KHRC ukiwa ikuluni lakini nguvu zako ziliambulia patupu

Pia Moi alijaribu lakini akashindwa, tafuta mpenzi mpate watoto ili huwe umeshikika uache kujisumbua na mambo yasiokuhusu." Mutua Alisema.