witchcraft

Wacheni Unyama! Mzee Wa Miaka 68 Auwawa Kwa Kukatwa Kwa Panga Kwa Tuhuma Za Uchawi

Polisi huko Voi kaunti ya Taita Taveta wameanzisha uchunguzi baada ya mzee mwenye umri wa miaka 68 kuuliwa kwa kukatwa kwa panga na watu wasiojulikana katika eneo la Bughuta kwa madai ya kushiriki uchawi.
 
Mkuu wa polisi Joshua Chesire anasema japo haijathibitishwa kiini cha mauaji hayo, wanakijiji wanasema mwendazake amekuwa akihusishwa na visa vya uchawi.
 
Visa vya wazee kuuliwa katika eneo hilo vimekithiri mno huko ikikadiriwa kuwa jumla ya watu 6 wameuliwa kwa tuhuma za uchawi katika kipindi cha miaka 3 iliyopita.
 
Chesire ameonya jamii dhidi ya kujihusisha na visa vya kuwashambulia wazee na badala yake kutafuta suluhu kutoka kwa viongozi wa serikali.
-Solomon Muingi

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments