EYDazKbWkAAX-N6.jfif

Wachezaji 4 wa Lokomotiv Moscow wapatikana na corona

Klabu inayocheza katika ligi kuu ya Urusi Lokomotiv Moscow imesema kuwa wachezaji wake wanne wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo.

Wachezaji hao  wanne ni  Dmitry Barinov, Anton Kochenkov, Timur Suleimanov na  Roman Tugarev ambao wametengwa ili kuzuia maambukizi zaidi.

Image

Taarifa hizi zinajiri saa chache tu baada ya Jefferson Farfan, mshambulizi wa klabu hiyo pia kupatikana na virusi hivyo mapema mwezi huu.

Baadhi ya wachezaji wengine sasa wamelazimka kusafiri hadi eneo lingine kujiandaa kwa kurejelea kwa ligi ya Urusi Juni 21, klabu hiyo imesema.

Image

Ligi ya Primia (EPL) inatarajiwa kurejea Juni 17

Kufikia Alhamisi, taifa la Urusi lilikuwa limesajili visa 379,051 vya maambukizi huku watu 4,142 wakiwa wamefariki.

 

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments