Wachezaji raga Wanyama, Olaba wahukumiwa miaka 15 kila mmoja gerezani

frank wanyama
frank wanyama
Wachezaji wawili wa raga Frank Wanyama na Alex Olaba hii leo wamehukumiwa miaka kumi na mitano kila mmoja gerezani kwa tuhuma za ubakaji.

Wawili hao walipatikana na hatia ya kumbaka mwanamuziki mmoja mwaka uliopita katika mtaa wa Highrise.

Hukumu hiyo inawadia hata licha ya wakili wao kuomba wasipewa hukumu ya jela.

Mahakama iliambiwa kuwa wachezaji hao wa timu ya Kenya Harlequin walimbaka mwimbaji huyo usiku mzima siku yake ya kuzaliwa katika manyumba ya Seefar mtaani Highrise, Nairobi, February 10 mwaka uliopita.

Wakili wa waili hao Wafula Simiyu aliambia gazeti la The Star kuwa hakimu mkuu Martha Mutuku aliamua kufuata ushahidi wake anayejitetea.

Katika hukumu yake, hamna yeyote aliyekuwa katika ile nyumba ispokuwa watatu hao. Hatua ya mshtakiwa kufuta kanda ya ngono waliyo tengeneza inaashiria hatia." Simiyu alisema.

Simiyu alisema kuwa Justice Mukumu aliamini ushuhuda wake mwanamuziki kuliko ushuhuda wa mshtakiwa.

Wakili huyo aliongeza kuwa hakimu alishikilia kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote ya kushiriki ngono.

Wachezaji hao wa Kenya Sevens wanapanga kukata rufaa.