soccer-apr-02-la-liga-villarreal-cf-at-fc-barcelona-390x285

Wachezaji wa Barca wagadhabishwa na jinsi klabu hiyo inamtaka Neymar

Wachezaji wa Barcelona hawana furaha baada ya klabu hiyo ya uhispania kutaka kuwatoza baadhi yao kwa klabu ya PSG ili wafaulu kumsajili  nyota wa Brazil Neymar.

Wachezaji hao walikuwa sawa na kurudi kwa Neymar katika klabu hiyo lakini walionekana wenye huzuni kwa kutumika kama ushawishi wa kumsajili nyota huyo.

Wachezaji ambao walikuwa wahamie PSG kwa minajili ya kumnunua Neymar ni Ousmane Dembele, Ivan Rakitic, Nelson Semedo, Arturo Vidal, na Jean-Clair Todibo.

Barcelona inatarajiwa tena kujaribu kumsajili Neymar, huku ikiripotiwa kuwa mbrazili huyo anataka kurudi Camp Nou pindi tu dirisha la kuhama litakapofunguliwa mwaka ujao januari.

Ililazimu Barca kupatia PSG wachezaji wake kadhaa baada ya kutumia billioni 13.7 pesa taslimu ya Kenya kumsajili Mfaransa Antoine Griezmann, kutoka klabu ya Atletico Madrid.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments