Wachezaji wa Uganda wamaliza mgomo baada ya kuahidiwa laki sita kila mmoja

Uganda.Cranes
Uganda.Cranes
Wachezaji wa Uganda waliregelea mazoezi yao ya kipute cha AFCON baada ya kuahidiwa kwamba watalipa dola elfu 6 zaidi kila mmoja, na nchi yao.

Kikosi hicho kiliwasilia uwanjani kuchelewa siku ya jumatano baada ya kuahidiwa pesa hizo. Wanatarajiwa kucheza na Senegal hii leo katika raundi ya 16 bora nchini Misri.

Hata hivyo timu hiyo iliregelea mazoezi jumatano kabla ya mechi hio saa nne usiku wa leo.

Shirikisho la soka Uganda limesema limeshalipa pesa zote walizokua wanadai wachezaji hao kulingana na mkataba wao, kabla ya kipute cha AFCON.

Katika mechi nyingine Morocco watachuana na Benin, huku wakitafuta kufika katika fainali ya AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2004.

Kwingineko, aliyekua wing’a wa Bayern Munich na Uholanzi Arjen Robben ametangaza kujiuzulu kwake kutoka soka. Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 35, amecheza mara 606 na kufunga mabao 210 katika tajriba yake ya miaka 19 na kushinda mataji kadha na Uholanzi, Uhispania, Ujerumani na Uingereza.

Huku Uingereza, Arsenal wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Malcom mwenye umro wa miaka 22, lakini azma yao kubwa ni kumnasa mshambuliaji wa Ivory Cost wa miaka 26, Wilfred Zaha kutoka Crystal Palace.

Gunners pia wana pauni milioni 70 wanapojianda kuweka dau la pili la kumnunua Wilifred Zaha, japo kuwa Palace wanamini thamani ya mshambuliji huyo ni pauni milioni 80.

Mchezaji Bruno Fernandes ameanza mchakato wa kuhamia Old Trafford. Nyota huyo wa miaka 24 anayecheza safu ya kati ya Sporting Lisbon na Ureno anatarajiwa kwenda Manchester kufanya vipimo vya afya.

Kwingineko Manchester City hawako tayari kulipa pesa zinazoitishwa na Leicester kumnunua Harry Maguire mwenye umri wa miaka 26, hatua ambayo imeipatia Manchester United nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza.

Tukirudi nchini, muogeleaji wa Kenya Emily Muteti alilazimika kukaa kwenye meli kwa siku tatu kabla ya mashindano ya kuogelea ya vyuo vikuu huko Napoli, Italia kwani hakua amesajiliwa. Muteti na waogeleaji wengine wawili wanaoiwakilisha Kenya Swaleh Talib na Ridhawan Abubakar walikosa kuhudhuria hafla ya ufunguzi ya mashindano hayo. Shirikisho la uogeleaji nchini halijasema lolote kuhusiana na suala hilo la hivi karibuni.