Wachezaji wanaolipwa mshahara mnono kutoka bara la Africa

Soka la bara Africa limekuwa katika hali tatanishi hasa ikifikia wakati wa kuwalipa wachezaji.

Hata hivyo, kunao wakali kutoka bara hili wanaokula mkwanja mrefu kwelikweli na hivyo kuishi maisha ya kifahari wanavyotaka.

Hatahivyo, wakali hawa hawachezi soka la Africa kwani wengi wao wamo ulaya ama Uarabuni.

Cedric Bakambu 300,000

Mshambulizi huyu anayetokea taifa la Congo DRC anaongoza orodha hii kwa kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi kwa wiki. Bakambu,anapokea mshahara wa pauni elfu mia tatu. Bakambu pia ndiye mchezaji ghali kutokea bara la africa baada ya kusajiliwa kwa euro sabini na nne kutoka vilareal ya Uhispania na Beijing Goun ya China.

Mohammed Salah 250,000

Sala anayekipigia Liverpool ya uingereza alishindwa kuipeleka taifa lake kwenye nusu fainali za Afcon anapokea mshahara wa pauni 250,000 kwaq wiki. Pharao huyWachezaji wanaolipwa mshahara Mnono kutoka bara la Africau alipata mkataba mpya na liverpool baada ya kuisaidia klabu hio kutwaa taji la klabu bingwa barani ulaya.

Piere Aubameyang 198,000

Mkali huyu kutoka taifa la Gabon anapokea donge nono la pauni elfu mia moja na tisini na nane kila wiki. Aubameyang, alimaliza akiwa mfungaji bora wa Arsenali msimu uliopita baada ya kucheka na nyavu mara ishirini na mbili. Aubameyang alijiunga na Arsenali akitokea klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani.

Idhion Ighalo

Ighalo anachezea klabu ya china,Yatai  analipwa mshahara wa 190,000 kila wiki. Ighalo alihamia uchina akitokea klabu ya Watford ya Uingereza na sasa analiongoza taifa lake la Nigeria kwenye michuano ya AFCON kule misri.

Riyad Mahrez na Naby Keita

Baada ya kujiunga na liverpool,Naby Keita anapokea mshahara wachezaji wanaolipwa mshahara Mnono kutoka bara la Africa pauni elfu mia moja na ishirini ilivyo kwake Riyad Mahrez anavyopewa na Manchester City. Wakali hawa wawili kutokea mataifa ya Guinea na Algeria wanayawkilisha mataifa yao kule nchini misri kwenye michuano ya AFCON.