matiangi

Waende!,Waziri wa Usalama Dr Matiang;i atia saini ya kuwasafirisha wachina wanne kwa lazima

Waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i alitia saini pendekezo la kuwafurusha kwa lazima wachina wanne walioonekana kwenye video wakimcharaza mkenya mmoja katika mkahawa wao eneo la Kileleshwa.

Tangazo hilo lilijiri baada ya mahakama kutoa amri ya kuzuiliwa kwa wanne kwa siku 15 zaidi kutoa  muda wa kufanyika kwa uchunguzi.Image

Picha ya siku: Mtindo mpya wa mavazi yake mama Diamond wafurahisha wengi

Wachina hao wanne wanakabiliwa na mashtaka ya kumuadhibu mmoja wa wakenya ambaye inadaiwa kuwa alifika kazini kama amechelewa ,video ambayo ilisababisha wakenya wengi kuingia mitandaoni na kukashifu kitendo hicho cha unyama.

Mwathiriwa ambaye hadi wa sasa juina lake halijabainika wazi,alieleza mahakama kuwa wafanyakazi wenza walikuwa walikuwa wanapitia kwa kichapo hicho iwapo wangechelewa kuripoti kazini kwa wakati ufaao akisema walikuwa wanahofia kupoteza ajira iliyokuwa inawapa kipato cha kila siku.

‘Shida ni kupata pesa!’ Joe Muchiri aomba msaada kumlipia Jowie dhamana ya millioni 2

Balozi wa Uchina nchini Wu Peng alikashifu tukio hilo akisema lazima wananchi wa Kenya waheshimiwe na watakaopatikana na makosa sheria ichukuwe mkondo wake.

Photo Credits: radio jambo

Read More: radio jambo

Comments

comments