Wafanya kazi wa JKIA kugoma huku safari za ndege kukatizwa

Katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta leo wasafiri wameweza kuona kizungumkuti baada ya safari za ndege kukatizwa kwa sababu ya wafanyakazi wa Kenya Aviation Workers Union(KAWU) kufanya mgomo wao.

Inasemekana kuwa wafanyakazi waliweza kugoma masaa kadhaa kabla ya Jumatano kufika,waliweza kueka vifaa vyao vya kazi chini na tangu masaa hayo hakuna ndege imeweza kutua wala kutoka katika uwanja huo wa JKIA.

Wameweza kugoma kwa kutoridhishwa na usimamizi wa bodi ya uwanja huo, na kuzungumza kuwa uwanja huo wa ndege utaweza kusimamiwa na Kenya Airways.

Usimamizi wa uwanja huo uliweza kuandikia wasafiri ujumbe kuwa wasiweze kuenda katika uwanja wa ndege kwa sababu wafanyakazi wamegoma.

"Kwa mgomo ambao unaendelea,wa wafanyakazi wa KAWU tunatarajia kukatizwa kwa ndege, wasafiri wa ndege za baada ya saa tano asubuhi wasiweze kuja katika uwanja wa ndege mpaka tuweze kuongea na kuwambia utaratibu,

Tunaomba msamaha kwa kutowajulisha kwa mapema," Kenya Airways walisema.

Kufuatia mgomo huo, JKIA imeweza kushushwa chini na wasafiri wengi kwa kuwaeka katika hali isiyojulikana na kuwachanganya.

Jumamosi asubuhi polisi waliweza kuwakimbiza wafanya kazi hao wa JKIA ili kuwatawanya, huku ikiwalazimu kutumia vitoa machozi ili waweze kutawanyika.

Foleni ndefu ziliweza kuonekana katika uwanja huo wa ndege, huku wasafiri wakisema kuwa wafanyakazi wengine wameweza kufunga lango kuu  ili wasiweze kuingia.

Wasafiri wengi hawakuweza kunyamaza bali waliweza kuandika mitandao ya kijamii wakieleza vile wameweza kukaa kwa muda mrefu katika uwanja huo.

Na hata wengine wakisema kuwa ndege zao zimechelewa na wengine kusema kuwa ndege zao zimekatizwa.

Ndege hizo zimeweza kuadhiri pia operesheni katika viwanja vya ndege vya Mombasa na Kisumu, mgomo huu unafuatia ilani iliyotolewa na wafanyakazi hao Februari 27.

Ni ilani iliyokuwa imeandikwa na wafanyakazi hao kupinga usimamizi wa uwanja huo kupewa Kenya Airways.

KAWU ina hukumu Kenya Airways kwa kuharibu pesa, katibu mkuu wa KAWU akiongea alisema kuwa sekta hiyo inaendelea kuwalipa maneja wa kubwa mshahara duni pamoja na wafanyakazi wa kawaida.