Wafanyakazi wa afya walioambukizwa virusi vya corona ni 634-CS Mutahi Kagwe

Waziri wa afya Mutahi Kagwe Jumatano alithibisha kuwa jumla ya wafanyakazi wa  afya walioambukizwa na virusi vya corona sasa imefikia 634.

Akiongea haya Mutahi alikuwa anatangaza maambukizi ya kila siku ya virusi vya corona, huku akisema kuwa idadi hiyo ya wafanyakazi wa afya imebeba asilimia 3% ya maambukizi ya corona humu nchini.

Hata hivyo, Mutahi aliwaonya wafanyakazi wa afya wanaoasi kutengwa kwa watu walioambukizwa.

"Tunawauliza wafanyakazi wa afya wafuate kanuni za wizara ya afya wao wenyewe, tunachua kuna baadhi yao ambao tabia zao hazipendezi

Kuna kesi ambayo tulikuwa nayo mmoja wa madaktari kutoka hospitali kuu ya Kenyatta ambaye alikuwa amesafiri na badala ya kuenda karantini alikuwa anataka kuenda thieta kufanya upasuaji lakini kwa bahati mbaya hakuweza

Tunamshukuru muuguzi aliyeripoti kesi hiyo, na hatua kali ilichukuliwa, hii wiki kuna daktari ambaye alipatikana na virusi vya corona na alikuwa anataka kukaa kikawaida kwa uaminifu hii ni tabia ya magaidi." Alizungumza Mutahi.

Hii leo watu 544 wamepatikana na virusi vya cororna huku 12 wakiaga dunia kutokana na virusi hivyo.