Wafanyakazi wawili katika shirika la utangazaji KBC wapatikana na corona

Wafanyakazi wawili katika shirika la utangazaji nchini KBC wamepatikana na virusi hatari vya corona.

Katika barua iliyotumwa kwa vyombo vya habari nchini na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Naim Bilal, amewataka wafanyakazi wengine kujitenga iwapo walitangamana na wale waliopatikana na virusi hivyo.

“Despite our good efforts, it has emerged that two of our staff have tested positive for COVID-19.“While appropriate protocols have been activated to prevent infection from the affected staff, the situation calls for enhanced personal responsibility within and outside BH to protect ourselves, colleagues, families and others,”  Bilal .

Vile vile, ametaka wale wanaohisi kuwa na matatizo yoyote kutafuta tiba katika maeneo ya afya nchini.