Wafanyikazi hao walibeba mabango walipokuwa wakindamana mbele ya hospitali hiyo huku wakionekana kupuuza kanuni ya kutokusanyika sehemu moja kwa wakati mmoja ingawaje wengi walikuwa wamevalia maski .
" Hatutakubali SRC kutuzungusha’ mmoja wao alisema wakisema wako tayari kwa lolote .
Katibu mkuu wa muungano wao Seth Panyako amesema wameamua kuufanya mgomo huo kwa sababu RC imeamua kujifanya kana kwamba ndio taasisi pekee nchini .
" Pesa ambazo tunazitaka tayari zimetolewa na kuidhinishwa . hakuna kurudi nyuma .Tunaitaka SRC itoe barua kwa KNH ikiishauri kutulipa pesa hizo na kisha tuufutilia mbali mgomo wetu’ amesema Panyako
Panyako amesema hazina ya kitaifa tayari imetoa shilingi milioni 601 ambazo bunge lilikuwa limeshaidhinisha .
"... Tatizo la pekee ni kwamba SRC haitaka KNH kutekeleza nyongeza ya mishahara . hatutakuwa na mazungumzo yoyote hadi tupate barua kutoka kwa SRC .