Wafisadi mtashikwa kwa siku chache - Uhuru ahaidi

Rais Uhuru Kenyatta jana aliweza kuahidi kuwa watakaopatikana na ufisadi na kashifa ya rushwa wataweza kukamatwa kwa siku chache zijazo.

Uhuru alisema kuwa wananchi wataweza kuona hatua zikichukuliwa kwa wale watakao kuwa wamepora mali ya umma.

"Wakenya wanahitaji hospitali, barabara, umeme na kazi, hilo haliwezi takelezwa kwa kupitia njia ya kukua tajiri haraka (get-rich-quick),

"Lakini kupitia jasho na kufanya kazi kwa bidii," Alizungumza rais Uhuru.

Rais Uhuru alisema kuwa kukomesha ufisadi ndio njia tu ya kipekee nchi inaweza kuendelea, aliongeza na kusema kuwa nchi haiwezi endelea kama mapato yanayokusanywa kwa wananchi yanaenda moja kwa moja hadi mifukoni mwa watu.

Uhuru alisema kuwa mtendaji alikuwa amejitahidi ili kusafisha ofisi ya Kurugenzi ya Uchunguzi wa makosa ya jinai (Directorate of Criminal Investigation).

Alisema kuwa ameweza kukumbusha mahakama kuwa wananchi wamechoka kuona watu wakiachiliwa kwa dhamana ndogo baada ya kuiba pesa nyingi za umma.

"Leo nilikuwa mkutano na mahakama ya juu na nimeweza kuwakumbusha wananchi wamechoka na wanawatazama,

"Niliweza kuwakumbusha kuwa tuliona mwanaume ambaye aliweza kutorosha mtoto wake kutoka hospitali ya Kenyatta kwa kushindwa kulipa deni,

"Nakushtakiwa siku yenyewe kisha kuachiliwa siku hiyohiyo kwanini tusifanye hivyo kwa wanao daiwa kuiba billioni za fedha kwa umma," Alieleza rais.

Rais aliweza kuwaambia kuwa wasiweze kungoja hadi pale wananchi watajichukulia sheria mikononi mwao.

Akiongea maneno hayo alikuwa eneo la Gitui kaunti ya Muraga wakati wa mazishi ya mwana biashara Kamau Thayu Kabugi.

Huku akimsifu na kusema kuwa mwanabiashara huyo alikuwa mwenye bidii na aliweza tia bidii kwa kazi yake kabla ya kuwa tajiri mkubwa.

"Alikuwa mfano mwema kwa familia na jinsi ya kuwa mwananchi mkubwa, hatungekuwa hapa kama si mfano mwema na heshima ambayo alionyesha katika maisha yake," Uhuru alinena.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga alisema kuwa  wameweza kuwa kama nchi ya biblia ya 'Sodoma na Gomorrah' kwa sababu ya kesi nyingi za kashfa ya rushwa na ufisadi.

"Tunapaswa kupigana na rushwa na ufisadi bila huruma wowote, ili nchi yetu iweze kuenda mbele kama nchi iliyo na huru," Raila alizungumza.

Alisema kuwa washukiwa wa rushwa wanapaswa kubeba msalaba wao wenyewe na wala wasiweze kuweka jamii zao hapo ndani.