Wagema Wa Chang'aa Waapa Kumpigia Raila Odinga Kura Kwa Imani Ataihalalisha Pombe Hiyo

chang'aa
chang'aa
Wagema, watumizi na wauzaji wa pombe haramu ya changaa kutoka mtaa wa motherland Mjini Webuye wamedai kwamba watampigia kura kinara wa NASA Raila Odinga atakayehalalisha matumizi na uuzaji wa pombe hio haramu.

Wakingozwa na Joseph Waliaula wamesema kwamba wamemskia Raila akisema kwamba ataweka mikakati maalum ya wao kuuza kinywaji hicho iwapo NASA Itabuni serikali ijao.

Walialua amesema kwamba ukosefu wa ajira na hali ngumu ya maisha imewalazimu kuuza pombe hio ili kupata mkate wao wa kila siku kando na kuwasomesha wanao.

Baadhi ya wakaazi wamedai kwamba maafisa wa polisi Webuye wamekua wakiwanyanyasa mara kwa mara badala ya wao kuwasaka waalifu walokithiri eneo hilo.

-Brian Ojamaa