Kenya imeongeza muda wa msamaha kwa raia wa kageni walio nchini bila vibali wakati huu wa janga la corona .
Mkurugenzi wa huduma za uhamiaji Alexender Muteshi kupitia taarifa kwa raia wote wa kigeni amesema wana wiki mbili kuondoka nchini .Muteshi amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kurejelewa kwa huduma za safari za ndege .
Amesema wale watakaoathiriwa wanafaa kupanga kuondoka Kenya katika kipindi cha iku 14 zijazo kuanzia septemba tarehe 14 au wachukue vibali vya kuruhuisiwa kuendelea kuishi Kenya .
Mwezi Mei Muteshi alitoa arifa ya kuwaagiza polisi kutokawakama raia wa kigeni walio nchini kinyume cha sharia . Alisema idara yake ilikuwa imepokea barua nyingi zilizotaka kujua hali ya raia wa kigeni waliokuwa wakiishi nchini .